Home Music Lyrics Emmanuel Mgogo – Uso Wangu

Emmanuel Mgogo – Uso Wangu

Uso Wangu by Emmanuel Mgogo MP3 MUSIC VIDEO

Uso Wangu LYRCIS by Emmanuel Mgogo:
Uso wangu utakwenda nawewe na wewe
Na mimi nitakupa raha raha
Uso wangu utakwenda nawewe na wewe
Na mimi nitakupa raha raha ah

Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe
Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe
Siwezi siwezi bila wewe siwezi

Kuna mahali natamani
Moyo wangu watamani nikae hapo
Niwe hapo daima

Mahali hapo kuna raha
Furaha na utoshelevu
salama amani vinatawala

Tena nasikia sauti ikiniambia mwanangu
Mahali hapo ni nyumbani ulipoumbwa ukae

Mahali hapo ni pale penye uwepo wa Mungu
Penye uso wa Mungu Baba

Mwanadamu Bila Mungu huwezi lolote
Hatuwezi lolote bila Mungu ni hasara

Musa kamwambia Mungu usituchukue toka hapa
Uso usipoenda nasi ee Mungu
Maana ni nini kitakachotutofautisha
Na watu wengine
Ni nini kitakachotufanya tushinde Bwana

Nena nasi Mungu, nena nasi Bwana
Usitutenge na uso wako nena nasi
Bwana twakuomba aah

Uso wangu utakwenda nawewe na wewe
Na mimi nitakupa raha raha
Uso wangu utakwenda nawewe na wewe
Na mimi nitakupa raha raha ah

Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe
Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe
Siwezi siwezi bila wewe siwezi

Siku moja bila Mungu bila uwepo wa Mungu
Ni sawa na miaka elfu jangwani
Siku moja bila Mungu bila uwepo wa Mungu
Ni sawa na miaka mingi jangwani

Hatua nyingi bila Mungu
Maendelea bila Mungu
Mwisho ni aibu ni bure eeh
Usianze wala kuenda bila Mungu
Hutafika mbali wewe mwite
Maana huwezi mwenyewe
Uso wa Mungu ukiwa nawe
Utakufanikisha wewe utakushindia
Utakuwa juu

Whatever comes in your way
You will overcome it
because the presence of the Lord is with you hey
Amesema kila anipataye mimi
Amepata uzima huyo
Na kibali kwa Bwana oh
Utapata zaidi ya hekima
Na elimu za dunia
Uso wa Mungu ukiwa nawewe utakuwa nuru

Tafuta sana kuwa na Mungu
Tunza sana uwepo wa Mungu
Maana huo ni ufungu wa Maisha

Ameahidi atakupatia ukimuomba lolote
Omba sana uwepo wa Mungu maishani mwako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here