Home Music Lyrics Goodluck Gozbert – Shukurani

Goodluck Gozbert – Shukurani

Shukurani by Gozbert MUSIC VIDEO

Shukurani LYRCIS by Gozbert:
Nina kushukuru Mungu sababu ya mengi, hata uhai huu sikustahili
Nina kushukuru Mungu tena sababu ya vingi, hata nikiwa nasali unajua namaanisha
Sio kama eti nilitenda wema wakuja linganisha na matendo yako makuu mimi Mungu ningekulipa nini
Ulikonitoa ni siri ya moyo wangu matopeni topeni ukaniketisha na wakuu juu
Umenipa heshima ukanifuta machozi asante ooh baba
Hata shukurani zangu ni kwako
Shukrani zangu ni kwako
Na shukurani zangu ni kwako

Shukurani zangu ni kwako, asante baba ooh
Aibu umefuta fedheha umefuta
Umenipa amani iliyo ya kweli nakumbuka nalia mimi ni yule ambae
Nilitukanwa na kwa dharau wakasema kwisha habari yake kuna kipindi nilikufa nikawa mifupa inayotembea
Ikiwa kwa siku za usoni walisema tunazika kesho
Ila kwa huruma uliniponya na kaburi kwa hurumaa na sitosahau wema wako wee baba
Hata shukurani zangu ni kwako
Shukrani zangu ni kwako
Na shukurani zangu ni kwako
Shukurani zangu ni kwako, asante baba ooh
Kama kusoma tumesoma wengi umeruhusu niwe na kazi nzuri
Ajali tulipata wengi umeruhusu nibaki nauzima (asante Baba)
Ndoa zilifungwa nyingi umeruhusu tubaki na amani
Furaha wanakosa wengi umeruhusu tabasamu kwangu
Na shukurani zangu

Yelele, yelele mama, yelele mama, yelele mama, yelele
Yelele, yelele mama, yelele mama, yelele mama yelele

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here