African Music Lyrics Kathy Praise – Mungu Wa Ishara

Kathy Praise – Mungu Wa Ishara

Mungu Wa Ishara by MP3 MUSIC VIDEO

Mungu Wa Ishara LYRCIS by Kathy Praise:
[In Swahili]

Mungu wa ishara
Moyo wangu ukuinue
Dhabihu yangu uipokee
Umetenda mambo makuu
Hakika wewe ni Mungu

Kama ulivyotenda hapo mwanzo
Tenda tena
Mungu mwenye nguvu, haushindwi kamwe
Tunakutazamia

Ulifufua wafu, na kuponya magonjwa
Vipofu wakapata kuona
Yote ukiyatenda, kwa utukufu wako
Yesu twakuabudu (Repeat)

Refrain:
Mungu wa ishara, Mungu wa miujiza, tunakuabudu
Mungu wa ishara, Mungu wa Miujiza, tunakuabudu

Wewe ni Mungu muweza yote, usiyeshindwa
Ishara zako twaona, nguvu zako twaona Yahweh!

Oh, Tenda tena Baba
Kama ulivyo ahidi, tenda
Tasa uwape watoto, tenda
Waliofungwa, kukataliwa, Jehovah, tenda
Waliyolaaniwa vunja laana, tenda Muujiza tukuone

(Refrain)

Wewe ni Mungu usiyeshindwa, tunakuabudu
Wewe ni Mungu usiyelala, tunakuabudu
Wewe ni Mungu usiyebadilika, tunakuabudu
Wewe ni Mungu muweza yote, tunakuabudu (Repeat)

(Refrain)

Leave a Reply