Najulikana Mbinguni by Martha Mwaipaja MP3 MUSIC VIDEO
Najulikana Mbinguni LYRCIS by Martha Mwaipaja:
Ninajulikana mbinguni
Ninaheshimiwa mbinguni
Nimehesabiwa na Yesu mwenyewe
Ananitosha milele
Ninajulikana kwa Baba juu
Ninaendelea tu na Yesu
Nimehesabiwa mbinguni juu
Amenipenda mimi, mwokozi
Sijajiweka mwenyewe mimi mwenzio
Nimewekwa na Mungu
Sijawahi jitambulisha mwenyewe
Nimetambulishwa na Baba
Walisemezena tusimtambulishe huyu
Nimetambulishwa mbinguni
Wakasema tusimchague
Nimechaguliwa mbinguni
Wakasema tusimkubali
Nimekubaliwa na Baba
Nimewekwa na Mungu Mwenyewe
Najulikana Mbinguni, najulikana mbinguni
Refrain:
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu
Unajulikana mbinguni rafiki ndugu yangu,
mbingu inakujua
Wametangaziana wasikusaidie,
umesaidiwa na Mungu
Wameabikizana wasikutendee,
umetendewa na Baba
Wamesama wakufute kwenye ukoo wao,
umeandikishwa mbinguni
Wamekataa kukutambulisha,
unatambulishwa na Mungu
Walisema hawatakutibu kabisa,
umeponywa na Mungu
Wamekataa kukubeba,
umebebwa na Yahweh
Wametamani ulie kila siku,
Baba kakukumbuka
Hujui vile nilivyo pendwa na Mungu!