Home African Music Lyrics Sifaeli Mwabuka – Mtukuze Mungu Tu

Sifaeli Mwabuka – Mtukuze Mungu Tu

Mtukuze Mungu by MP3 MUSIC VIDEO

Mtukuze Mungu LYRCIS by Sifaeli Mwabuka:
Natamani kusema na wewe hapo ulipo
Shauku yangu nizungumze na wewe
Kama unanisikia
Oooh natamani kusema na wewe hapo ulipo
Shauku yangu nizungumze na wewe kama unanisikia

Vile ulivyo ni mpango wa mungu uwepo
Ana makusudi na wewe ndio maana upo leo
Unavyojitazama hivyo ulivyo
Ni mpango wa mungu kwako ndio maana uko hivyo

Vile ulivyo ni mpango wa mungu uwepo
Ana makusudi na wewe ndio maana upo leo
Unavyojitazama hivyo ulivyo
Ni mpango wa mungu kwako ndio maana uko hivyo

Wengine wamekufa hatujui tutaonana lini
Wewe uko hai mtukuze mungu tu
Wengine wanalia hawajui wataishi vipi kesho
Wewe una kula na kunywa mtukuze mungu tu

Wengine wamelazwa hawajui watapona lini
Wewe uko na afya mtukuze mungu tu
Wengine wamepoteza baadhi ya viungo vyao
Wewe uko mzima mtukuze mungu tu

Wewe simama, simama
Simama mtukuze mungu tu
Wewe simama, simama
Simama mtukuze mungu tu

Vile ulivyo
Simama, simama

Kwenye taaabu zako
Simama, simama
Kwenye mateso
Simama, simama
Kwenye mapito yako
Simama, simama
Mtukuze mungu tu

Mtukuze yesu
Simama, simama
Mtukuze baba
Simama, simama
Yahweh, yahweh, yahweh
Simama, simama
Mtukuze mungu tu

Ni kweli umepitia magumu yenye kukuvunja moyo
Mungu wako anajua jinsi ulivyo
Ni kweli ulilia sana hujui mwisho wakweli
Mungu wako anajua kilio chako

Ni kweli umepitia magumu yenye kukuvunja moyo
Mungu wako anajua jinsi ulivyo
Ni kweli ulilia sana hujui mwisho wakweli
Mungu wako anajua kilio chako

Jaribu lako limekuwa kama mlima
Wewe usirudi nyuma mtukuze mungu tu
Watu watasema kama vile kwa ayubu
Usinyamaze kimya mtukuze mungu tu

Jaribu lako limekuwa kama mlima
Wewe usirudi nyuma mtukuze mungu tu
Watu watasema kama vile kwa ayubu
Usinyamaze kimya mtukuze mungu tu

Wewe simama, simama
Simama mtukuze mungu tu
Wewe simama, simama
Simama mtukuze mungu tu

Vile ulivyo
Simama, simama
Simama mtukuze mungu tu

Kwenye taaabu zako
Simama, simama
Kwenye mateso
Simama, simama
Kwenye mapito yako
Simama, simama
Simama mtukuze mungu tu

Mtukuze yesu
Simama, simama
Mtukuze baba
Simama, simama
Yahweh, yahweh, yahweh
Simama, simama
Simama mtukuze mungu tu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here