Home African Music Lyrics Sifaeli Mwabuka – Niko Hapa Baba Niguse

Sifaeli Mwabuka – Niko Hapa Baba Niguse

Niko Hapa Baba Niguse by MP3 MUSIC VIDEO

Niko Hapa Baba Niguse LYRICS by Sifaeli Mwabuka:
Najua Baba macho yako yanaona
Nitazame na mimi
Najua Baba masikio yako yanasikia
Sikia maombi yangu

Ni wengi wamekuona Baba ukijibu
Jibu na mimi
Oh ni wengi wamekuona Baba ukitenda
Tenda kwangu na mimi

Ni wewe Mungu wangu usiyenaupendeleo
Niguse na mimi Baba
Ni wewe Baba usiyenaupendeleo
Nikumbuke na mimi

Niko hapa, niko hapa
Niko hapa Baba uniguse

Niko hapa, niko hapa
Niko hapa, Baba uniguse

Najifunza kwa wengine walionitangulia
Nafahamu wewe unatenda
Najifunza kwa Yakobo
Hakukuacha Baba uende
Aling’ang’ana na wewe
Akasema huwezi kwenda usiponibariki
Yakobo na aseme
Akasema huwezi kwenda usiponiponya
Akashika pindo lako yule mwanamke

Na mimi niko hapa
Niko hapa, niko hapa
Niko hapa Baba uniponye
Niko hapa, niko hapa
Niko hapa Baba uniguse

Niko hapa, niko hapa
Niko hapa, Baba uniguse

Leave a Reply